TANZANIA YA KISWAHILI: MAKONDA ATANGAZA NEEMA YA VIWANJA/HOTUBA: RC MAKONDA ASHUSHA NEEMA KWA WATUMISHI WA UMMA DAR ES SALAAM HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM KWA WATUMISHI WAKE NA WANANCHI WA MKOA ...
Monday, September 18, 2017
Wednesday, September 6, 2017
INIESTA ATAKA KUONDOKA BARCA
ANDRES INIESTA NA MKATABA MPYA
Mchezaji nguli wa barcelona ANDRES INIESTA amefikilia kutoongeza mkataba tena na magwiji wa Hispania Barcelona Hata hivyo,ANDRES INIESTA alionekana katika uwanja wa ndege wa El Prat kutoka Hispania siku ya Jumatano,Baada ya kuulizwa maswali na mwandishi Iniesta aliwaambia waandishi wa habari "hapana" wakati alipoulizwa kama angeweza kuthibitisha kuwa kama kuna makubaliano yoyote .Bartomeu amesema: "Sisi tuna makubaliano ya msingi kwa Iniesta kuanzisha upya [mkataba wake] na tunatarajia kumaliza wiki hizi zijazo. Tunasubiri kuendelea na Mazungumzo, lakini Iniesta ni mchezaji tunataka amalizie soka lake Hapa na anahisi ni wakati mzuri wa kustaafu.
Bartomeu amesema: "Sisi tuna makubaliano ya msingi kwa Iniesta kuanzisha upya [mkataba wake] na tunatarajia kumaliza wiki hizi zijazo. Tunasubiri kuendelea na Mazungumzo, lakini Iniesta ni mchezaji tunataka amalizie soka lake Hapa na anahisi ni wakati mzuri wa kustaafu.
NDOTO ZA CAMERRON KOMBE LA DUNIA
DALILI MBAYA KWA CAMEROON :URUSI 2018
Timu ya taifa ya soka ya Cameroon itamenyana na Nigeria baadaye Jumatatu jioni katika mechi muhimu ya kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Mchuano huu unachezwa jijini Yaounde. Wiki iliyopita, wakiwa ugenini, Cameroon walifungwa mabao 4-0 na wenyeji wao Nigeria.
Kuelekea katika mchuano huu, kocha wa Cameroon Hugo Broos ameonekana kukata tamaa na kusema kuwa hakuna matumaini ya kufuzu katika fainali hiyo.
Broos amesema vijana wake watajitahidi sana kucheza vema ili kulinda heshima yao nyumbani lakini sio kufuzu katika michuano hiyo.
“Mechi hii sio muhimu kwetu ili kufuzu kucheza kombe la dunia lakini tunachotaka ni kulinda heshima yetu,” alisema.
Ikiwa Cameroon inataka kufuzu itabidi ishinde mechi zake zote tatu zinazosalia na kuomba kuwa Nigeria nayo ipoteza mechi zote zinasalia, kitu ambacho hakitawezekana.
Nigeria wanaongoza kundi la B kwa alama 7 baada ya mechi tatu, Zambia ikiwa ya pili kwa alama 4 huku Cameroon ikiwa ya tatu kwa alama 3 huku Libya Algeria ikiwa ya mwisho kwa alama 1.
TETESI ZA ULAYA:FIFA Vs. UINGEREZA
Fifa na michakato ya Kuiondoa Uingereza katika Kombe la Dunia
Hofu imeanza kutanda kwa mashabiki wa soka nchini humo jambo hili linaweza kuwatoa Uingereza katika michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Russia ,Endapo bunge litapiga kura wiki ijayo basi itaiweka Uingereza katika hali ya sintofahamu juu ya ushiriki wao katika kombe la dunia la mwaka 2018.
Mgogoro kati ya bunge la Uingereza na FA unakuja baada ya baadhi ya viongozi wa zamani wa FA kudai kwamba chama hicho kinashindwa kujiendesha.Katika barua ambayo viongozinwa zamani wa FA walimuandikia mwenyekiti wa kamati ya michezo bungeni bwana Damians Collin inaelezwa kwamba FA imekwama na imeshindwa kujiendesha.Inasubiriwa kwa hamu kuona nini kitatokea baada ya kikao cha bunge la Uingereza kutoa maamuzi yao kuhusu FA.
Kesi hii ya Uingereza haina utofauti na kesi iliyokuwa ikiwakabili Kuwait katika hatua ya kushiriki kombe la dunia 2018.Serikali ya Kuwait iliingilia masuala ya soka nchini humo.Wakiwa wamefika raundi ya tatu ya mechi za kufuzu kombe la dunia FIFA waliamua kuwatoa Kuwait katika mashindano hayo baada ya serikali yao kukiuka sheria za Fifa.
Uingereza ambao hadi sasa wako katika nafasi nzuri ya kufuzu kombe la dunia kwani wanaongoza kundi lao la F. Uingereza wamebakiza mechi 6 tu kufuzu kombe la dunia lakini sheria za FIFA zinaweza kuwazuia kufuzu ama kuendelea na mechi zao kwa sasa.